Hansard Summary

Sentimental Analysis


THE PARLIAMENT OF KENYA

NATIONAL ASSEMBLY

THE HANSARD

Hon Members, we do not have the requisite numbers. I order that the Quorum Bell be rung for five minutes. (The Quorum Bell was rung) Order, Hon. Members! When the Quorum Bell is being rung, you should not walk out of the Chamber. I want to ask those Members who are walking out to please adhere to the Standing Orders. Hon. Members, I can confirm that we now have the numbers to start the session.
Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamkunji. Lengo lake ni kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Lugha yetu ya Kiswahili ni safi. Itakuwa vyema lugha za Kiswahili na Kiingereza zikienda sambamba. Mambo mengi tunayoyafanya tunahitaji lugha itakayotuwezesha kufanya shughuli kadhaa wa kadha; haswa za kimasomo, kibiashara na kimatibabu. Mimi, kama daktari, mara nyingi napenda mgonjwa anieleze kuhusu ugonjwa alionao kwa lugha ambayo anaifahamu vizuri. Kuna watu ambao wanapoongea wanatumia lugha isiyoeleweka. Kizazi cha sasa kinatumia lugha ya mtaa ambayo inaitwa Sheng. Rafiki yangu, Mhe. Babu Owino na jirani yangu Mhe. Caleb Amisi, wanaongea lugha ya Sheng. Hawa vijana lugha yao ni sheng. Hivyo ndivyo tunapoteza lugha yetu ya Kiswahili. Lugha ya Sheng haieleweki miongo mwa Wakenya wengi na watu kutoka mataifa jirani. Inasemekana Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar… Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Mbunge wa Embakasi Mashariki. Mhe. (Daktari) Robert Pukose (Endebess, UDA): Ni Mbunge wa Embakasi Mashariki, Mhe. Spika wa Muda. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Okay. Mbunge wa Embakasi Mashariki. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 16 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Mhe. Babu Owino (Embakasi Mashariki, ODM): Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nilikuwa nimekuomba nafasi nilete hoja ya nidhamu lakini siwezi... Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Ni Hoja ya Nidhamu. Mhe. Babu Owino (Embakasi Mashariki, ODM): Siwezi kukulaumu, Mhe. Spika wa Muda. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Inabidi utuambie unaleta hoja ya nidhamu chini ya Kanuni gani. Mhe. Babu Owino (Embakasi Mashariki, ODM): Ahsante sana. Mhe. Spika wa Muda, Mhe. Pukose amesema mimi huongea Sheng, ambayo ni lugha isiyoeleweka. Nataka kukuambia kwamba leo hii nimejawa na bashasha, mpekwempekwe, chakari za kungulu… (Kicheko) Maanake tunatukuza Kiswahili lakini nimeona Wabunge wengi hapa hawaelewi hii lugha. Kwa hivyo, ni muhimu sana Wabunge warudi shule ili wasome lugha ya Kiswahili. La mwisho… Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Mhe. Babu Owino, inafaa utueleze ni Kanuni gani ambayo unaeleza. Mhe. Babu Owino (Embakasi Mashariki, ODM): Nataka kujibu mwenzangu kwa sababu amesema mimi huongea Sheng. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Utamjibu nikikupatia nafasi ya kuchangia, tafadhali. Mhe. Babu Owino (Embakasi Mashariki, ODM): … (Aliongea nje ya rekodi) Mhe. (Daktari) Robert Pukose (Endebess, UDA): Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Lahaja ambayo Mhe. Babu anaongea ni Kiswahili ambacho hakijakuzwa kwa njia safi. Wanasema Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar na Tanzania. Kililelewa hapa Kenya, kikakufa kule Uganda na kikazikwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mimi ni jirani wa nchi ya Uganda. Kwa sasa, wameanzisha Kiswahili katika shule za msingi na sekondari. Kwa hivyo, Kiswahili kinaendelea kuamka sasa. Mhe. Hassan ameleta Hoja hii wakati unaofaa. Tukiwa na Baraza la Kiswahili la Kenya litashughulikia suala la kukizuza Kiswahili, na sio kulazimisha Kiswahili kitumike mahali ambapo hakifai. Baraza hilo litahakikisha kwamba Kiswahili kinachotumika ni nadhiri ama kinakubalika na kila mtu. Kiswahili kilibuniwa kutoka kwa lugha za kibantu na Kiarabu. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba Kiswahili tunachotumia ni sanifu, ili kitumike kwa mambo yote. Jamii zingine zinatumia Kiswahili ambacho ni tofauti. Kwa mfano, majirani wangu kama Mhe. Kalasinga hapa, akitaka kusema anaenda, anasema “naendako” ama “nakujako”. Hapa unaona lugha ya Kiswahili haitumiwi vizuri. (Kicheko) Sisi, majirani wa Mhe. Kalasinga, tunaelewa akisema “ninakujako bwana”. Tunafahamu anakuja na anasema kwa njia nzuri. Lakini, mtu kutoka sehemu nyingine hataelewa. Tulipohudhuria michezo kule Tanzania, Wakenya tunapenda kusema ‘nipe’ kitu fulani, lakini Watanzania kwa lugha yao wanasema “tafadhali naomba”. Wakenya hatutaki kusema hivyo. Sisi tunasema “lete hii” na tunaona sio madharau. Lakini ukiambia Mtanzania “leta hii” hata kama ni kwa duka, anaona kama unmadharau. Kwa hivyo, ni lazima tujaribu kutumia Kiswahili sanifu, na kwa njia ambayo ni ya heshima, ili kila mtu aridhike katika nchi yetu. Sitaki kusema mengi sana. Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii. Natarajia kwamba ataenda zaidi ya hapo na kutengeneza Mswada ambao tutaujadili na Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 17 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. kuupitisha hapa Bungeni ili uweze kuwa miongoni mwa Sheria za Kenya. Tukifanya hivyo, tutaliwezesha Baraza la Kiswahili lililopendekezwa hapa kufanya kazi ambayo tunaizungumzia. Tunapoileta kama Hoja sasa hivi, hatujafanya chochote. Pale tumeonyesha maoni ama nia yetu ya kufanya hayo. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Ahsante, Mhe. Pukose. Nafasi hii ni ya Mhe. Abdul Haro kutoka Mandera Kusini. Mhe. Abdul Haro (Mandera Kusini, UDM): Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa adimu niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa bungeni na Mhe. Yusuf Hassan, ambaye namshukuru sana. Hoja hii inaihimiza Serikali, kupitia vyombo vya dola husika, kuanzisha Baraza la Kiswahili. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu ya mambo kadhaa ambayo baadhi ya Wabunge wenzangu wamegusia. Mbali na kuwa lugha pekee ya Kitaifa, lugha ya Kiswahili pia huwa inatumiwa kama nembo ya umoja wa taifa, ama symbol of national unity kwa Kimombo. Pia lugha hii inazungumzwa na Wakenya wengi, hasa wale ambao wanaishi kule mashinani. Umuhimu wa Baraza la Kiswahili ambalo tunahimiza kubuniwa kupitia Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan sio tuu litasaidia kukuza uenezaji wa uzungumzaji wa Kiswahiki katika Taifa hili, bali pia litasaidia katika kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili sanifu katika shule zetu. Tusisahau kwamba somo la Kiswahili linahitajika, hasa wakati wanafunzi wanapotaka kuendelea na masomo katika taaluma zingine za juu. Kwa mfano, wanafunzi ambao wanataka kujifunza taaluma ya Kiswahili, somo la Kiswahili ni muhimu. Ni lazima uwe umefanya vizuri katika Kidato cha Nne ili uweze kuingia katika taasisi za kufunza taaluma ya ualimu. Hata wale ambao ni mawakili, tunafahamu kwamba lugha ya Kiswahili inahitajika katika taaluma hiyo. Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya kusaidia kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Litakapobuniwa, Baraza hilo litachangia ukuzaji wa Kiswahili katika kuzungumza na pia itahimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli za kila siku serikalini. Kwa mfano, Bunge ama wizara za Serikali muhimu, zitatumia lugha ya Kiswahili kwa sababu hii ndiyo lugha ambayo inatumiwa na Wakenya wengi katika mawasiliano yao ya kila siku. Baraza la Kiswahili litasaidia kuhimiza matumizi ya Kiswahili sanifu katika taasisi zetu zote za elimu na ofisi zetu kama vile Bungeni na kwenye idara zinginezo. Baraza la Kiswahili pia litasaidia katika kutafsiri. Kwa mfano, litatafsiri ripoti ambazo zinatoka katika taasisi fulani, vitabu na pia sera za Serikali ambazo zinaweza kutumika mashinani na kueleweka vizuri na wananchi wetu wengi ambao wanategemea kuzungumza lugha ya Kiswahili. Baraza la Kiswahili likibuniwa litasaidia kutoa huduma za tafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Ninafurahi kwa sababu lugha ya Kiswahili inazungumzwa na wananchi wengi katika kanda ya Afrika Mashariki, ambako tuko. Pia, ni lugha rasmi ambayo inazungumzwa katika Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Kwa hayo machache, Mhe. Spika wa Muda, namshukuru tena Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng): Asante sana. Nafasi hii itaenda kwa Mhe. Amos Mwago wa Starehe. Mhe. Amos Maina (Starehe, JP): Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia Hoja hii kuhusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa letu la Kenya. Kwanza kabisa, namshukuru na kumpongeza mshauri wangu wa kisiasa, Mhe. Yusuf Hassan, ambaye ni jirani yangu kutoka eneo Bunge la Kamukunji. Ameleta Hoja hii Bungeni kutokana na yale ambayo tunapitia kama Wabunge wa eneo hili la Nairobi. Eneo hili la Nairobi lina changamoto kubwa sana katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu, hapa Nairobi lugha ya Sheng imeweza kukoloea sana na ikawa ndio inatumika kwenye mitaa. Kwa kiwango kikubwa, mawasiliano ni kikwazo wakati wananchi tunaowakilisha wanataka huduma za Serikali. Kuna idadi kubwa ya watu ambao Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 18 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. hawajaenda shule na hawafahamu Kiingereza. Lugha mbadala ya kuweza kupata usaidizi katika ofisi ya Serikali ni lugha ya Kiswahili. Wananchi wanakuwa na changamoto kubwa, hasa vijana wenye umri mdogo ambao wanatumia Sheng, wanapokuja kwenye ofisi zetu kutafuta usaidizi. Ukiangalia pia kwenye sehemu zetu za uchuuzi, idadi kubwa ya wachuuzi ni watu ambao hawakuenda shule na hawafahamu Kiingereza. Wakienda sokoni kufanya biashara zao, wengi wao huenda na lugha ya asili kama vile Kikuyu, Kiluo, Kiluyhia na Kinandi. Wakiwa pale sokoni, inakuwa vigumu kufanya biashara kwa sababu hakuna lugha moja ambayo watu wanaweza kutumia kuwasiliana kuhusu mambo ya uchuuzi. Kulingana na mimi, Baraza la Kiswahili likibuniwa na Kiswahili kikiendelea kukuzwa, itakua ni njia moja ya kusaidia mawasiliano kwenye nafasi zetu za kazi. Mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf. Sheng ni lugha ambayo itakuja kunoga hapa Nairobi na huwa inabadilika kila mara. Wakati huu wanaongea hivi lakini baada ya miaka mitano, itakuwa imebadilika kwa kasi kikubwa sana. Kwa mfano, kitambo tulikuwa tunamuita Mhe. Yusuf kule mtaani bazenga lakini siku hizi vijana wanamuita mzimbitim. Hivyo ni vitu viwili ambavyo havieleweki. Lugha ya Sheng inafanya uhusiano kati ya wazazi na watoto wao kuwa mgumu. Hata kama watoto wanapanga mabaya, utakua katika maongezi yao lakini hutaelewa neno hata moja. Ukiangalia pia upande wa utamaduni, wakati tulipokuwa tukienda shuleni, tulikua na ubunifu wa hali ya juu katika sanii na uigizaji. Tulikuwa tunaona michezo mingi ya utamaduni kutoka kule Pwani. Kwa mfano, hivi majuzi kumekuwa na mchezo wa kuigiza uliokuwa ukiendele kwenye runinga, kuhusu Mekatilili wa Menza – ambao ulikuwa na mafunzo mengi sana ya utamaduni wa Mijikenda. Watu wengi walipitwa na utamaduni huu kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Itakuwa jambo la muhimu sana tukibuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kurudisha ubunifu wa kitambo. Hii ni kama vile fasihi na michezo ya kuigiza zilivyokuwa, ili nchi yetu iweze kuendelea mbele vizuri. Kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, nimekuwa mfanyibiashara Tanzania, Uganda, Congo, na kadhalika. Changamoto kubwa imekuwa ni mawasiliano. Mawasiliano kwenye biashara imekuwa ngumu sana kwa maana Kiswahili kinachotumika Uganda na Tanzania ni tofauti sana ni kile cha Congo. Ukiangalia historia, utapata kuwa asili ya Kiswahili ni Kenya. Lakini mataifa jirani yameweza kuchukulia Kiswahili kwa umaarufu mkubwa zaidi. Kwa mfano, hata Rais wa kule Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati wa mazishi ya marehemu Mhe. Magufuli, alisema kuwa ataanzisha somo la Kiswahili katika shule za nchi yake. Lakini upande wetu, Kiswahili hakitiliwi maanani sana ilhali ni lugha ambayo imetupa umaarufu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukiweza kubuni Baraza la Kiswahili, naamini tutaweza kupata maprofesa kama Ali Mazrui, ambaye alipata umaarufu wake kwa kukuza Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inahifadhi sana mambo ya nidhamu. Inasemekana kuwa ukiongea lugha ya kigeni, unaongea kutoka kwa ubongo lakini ukiongea lugha ya asili unaongea kutoka kwa roho yako. Ndio maana kuna maneno ambayo unaweza kutumia rahisi sana kwa lugha ya Kiingereza lakini maneno hayo huwezi kusema mbele ya watu ukitumia lugha ya Kiswahili. Sitaki kutoa mfano lakini ni rahisi sana kusema kwa Kiingereza yale maneno ambayo tunasema ni wasio wa maadili lakini kwa Kiswahili inakuwa ni vigumu. Hii ni kwa sababu Kiswahili ina nidhamu zake. Ukiangalia pia kwa mitandao ya kijamii, kwa sasa hivi, lugha ya Kiswahili iko hali mahututi. Hii ni kwa sababu kwenye mitandao yote ya kijamii, kama vile WhatsApp, kama alivyosema Mhe. Didimus Barasa, kila mtu anatumia lugha ya Kimombo. Inaweza kuwa vyema Baraza la Kiswahili liweze kuangazia mambo kama hayo ili tuweze kurudisha umaarufu wa Kiswahili. Kwa hayo mengi, Mhe. Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Naomba kumpa dadangu dakika zilizobaki. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 19 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Asante sana. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng): Mhe. Mwago, hauna dakika za kumpa mtu. Nafasi hii itamwendea Mhe. Mwangale Chiforomodo na atafuatwa na Mhe. Martha Wangari. Iwapo Mhe. Chiforomodo hayupo, nafasi ni ya Mhe. Paul Mwirigi. Mhe. John Paul Mwirigi (Igembe Kusini, UDA): Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii. Kabla ya kutoa maoni yangu, nachukua fursa hii kuwashukuru wananchi wa Igembe Kusini kwa kunipa nafasi ya pili ya kuwawakilisha. Wengi walidhani kuwa sisi vijana hatuna ubunifu wa kufanya kazi na kuwasaidia wananchi. Wengi walidhani kwamba nitakuwa kiongozi wa muhula mmoja tu na baada ya hapo nitasahaulika. Nawashukuru sana wananchi wa Igembe Kusini kwa kunipa nafasi ya pili ili niweze kuwahudumia. Kama nilivyowaambia, nitawahudumia kwa uaminifu na kutenda kazi zaidi ya vile nilivyofanya katika muhula wa kwanza. Kwa hivyo, nawashukuru sana na naomba Mungu aweze kutupa nguvu kwa miaka hii mitano ili niweze kuwahudumia vyema. Mhe. Spika wa Muda, nampa kongole Mhe. Yusuf kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Unafahamu vyema kuwa lugha ya Kiswahili imedhalilishwa sana katika taifa hili ilhali tunajua kuwa ni lugha ya kitaifa na pia imekubalika katika Katiba yetu kutumika kama lugha rasmi. Kwa hivyo, kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa hili kutachangia pakubwa kuhakikisha kwamba lugha hii imeweza kupata nafasi yake katika taifa hili. Huwa tunasema kila wakati kuwa taifa letu limejengeka katika Kiswahili lakini wakati ambapo tunaenda katika mikutano mikuu, tunaendelea kutumia lugha ya wakoloni bila sisi wenyewe kujielewa kwamba tuko na lugha na utamaduni ambao tunafaa kuhifadhi. Baraza la Kiswahili likibuniwa, litasaidia taifa letu kushiriakiana kwa pamoja na pia kuleta umoja. Wakenya wakizungumza lugha moja na kutupilia mbali lugha za makabila yao, hii lugha itakuwa ni ya kuleta umoja. Wakenya wote tutakuwa kabila moja kwa maana wataunganishwa na hii lugha, itatusaidia pakubwa na itainua na kuimarisha utaifa wetu. Naibu Spika wa Muda, ninampongeza Mhe. Yusuf kwa kuleta hii Hoja Bungeni. Ninaiomba Wizara husika kuangazia na kutilia mkazo suala la kubuniwa kwa baraza lililopendekezwa punde tu Bunge litakapopitisha Hoja hii. Tutakapoipitisha hii Hoja, Serikali iichukulie kwa uzito ili iweze kuwasaidia wananchi. Vilevile, ningeomba sana Wakenya, na haswa taasisi za elimu, watumie lugha ya Kiswahili ili waimarishe utamaduni wetu na pia wanafunzi waweze kuelewa nchi hii imetoka wapi na inaelekea wapi. Wanafunzi wanafaa kuelewa kuwa hii si nchi ya ukabila kwa maana watakuwa wameunganishwa na lugha ya Kiswahili. Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili ni jambo ambalo limechelewa sana na huu ni wakati mwafaka wa kulitekeleza jambo hili. Baadhi ya Wabunge wenzangu wamesema kuwa tulipokuwa tukiomba kura, tulitumia lugha ya Kiswahili. Tuliwasiliana na wananchi moja kwa moja na walituelewa. Sio vyema basi kila wakati kutumia lugha ya mkoloni, ambayo mwananchi haelewi. Kuna pendekezo kwamba lugha rasmi ya Kiingereza iwe inatumika kutoka Jumatatu mpaka Ijumaa. Ni vyema kuhimiza matumizi ya Kiswahili. Vilevile, Baraza la Kiswahili litakapobuniwa litasaidia mpaka vyombo vya habari. Lugha zinazozungumzwa kwenye vyombo vya habari sio sanifu. Baadhi ya wazungumzaji wanaharibu lugha. Baraza lililopendekezwa litasaidia kuwalazimisha wahusika kwenye vyombo hivyo kusanifisha lugha ya Kiswahili. Baadhi ya Wabunge wamegusia suala la vijana wanavyotumia lugha ya Sheng. Hili baraza litakapobuniwa, tutaweka kanuni mwafaka ili kutoa mwelekeo kuhusu matumizi ya Kiswahili. Hii lugha itajengeka vyema katika taifa hili na itasaidia kukua kwa hili taifa. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 20 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Waheshimiwa Wabunge, ningependa kuwaeleza kwamba aliye juu kwenye orodha yangu ni Mhe. Martha. Mtu yeyote asiseme nimemkatiza. Alitangulia kufika Bungeni. Mhe. Martha Wangari (Gilgil, UDA): Asante Mheshimiwa Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii. Ninampa kongole Mhe. Yusuf Hassan wa Kamukunji kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Nafikiri leo ni mara ya kwanza sisi wenyewe kuendeleza mazungumzo na mjadala karibu kikao kizima cha asubuhi tukitumia lugha hii ambayo tunaienzi. Sisi sote tumeweza kusoma mambo mengi. Tumeona kwamba baadhi yetu tumeshindwa kutumia dakika kumi tulizotengewa kuchangia Hoja hii. Hakuna hata mmoja wetu aliyewashiwa taa nyekundu wakati anapozungumza, kuashiria kumalizika kwa muda wake. Hii ni kwa sababu hatuna uzoefu wa kutumia hii lugha. Tunafaa kuwa kwenye mstari wa mbele kuendeleza na kuonyesha vile lugha ya Kiswahili inafaa kutumika. Mambo na historia ya Kiswahili yanajulikana tangu zamani. Lugha hii imetumika haswa kwenye taifa la Tanzania. Marehemu Mwalimu Julius Nyerere aliweza kutumia Kiswahili sana Tanzania ilipokuwa ikipigania uhuru kupitia chama cha TANU. Hatimaye, UNESCO ilitenga tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya ya kusherehekea Kiswahili duniani. Idadi ya watu wanaotumia Kiswahili ulimwenguni ni zaidi ya milioni mia mbili. Uzuri ni kwamba hili jambo limeweza kuchukuliwa kuwa la maana sana na UNESCO, ambayo imeidhinisha Kiswahili kitumike kama lugha ya kiasili na utangamano duniani. Hapa Kenya, tumeweza kuwa na utangamano wa jamii tofauti. Tumewahimiza watu kutoka jamii tofauti hata waweze kuoana na tumepoteza lugha zetu za kiasili. Lugha ambayo imebaki ni Kiswahili – ambayo inatuunganisha sisi sote. Baadhi ya Wabunge wenzangu waliotangulia kuchangia Hoja hii, wamesema kwamba wakati tulipokuwa tunapiga siasa muda usiokuwa mrefu, hatukuwa tunatumia sana lugha ya Kizungu. Tulitumia Kiswahili. Wakati unahudhuria mchanganyiko wa jamii nyingi unafaa kutumia lugha ya kiasili. Kwa mfano, ukihudhuria mkutano wa Wakikuyu, unafaa uongee Kikuyu. Unapohudhuria mkutano wa Wajaluo, unaongea Dholuo ama Kijaluo. Lakini unapokwenda kwenye mkutano unaohudhuriwa na mchanganyiko wa jamii tofauti, kama vile Wakisii, Wajaluo na Wakalenjin, itabidi utumie Kiswahili ndiyo muweze kuongeleshana na kusikilizana. Hapa Bungeni, tumeonyesha kuwa hii lugha inawezakutumika. Pia, tumeitumia lugha katika Kanuni za Kudumu za Bunge ama National Assembly Standing Orders. Nchini Tanzania, majina ya taasisi za umma na wizara za serikali yamenukuliwa kwa Kiswahili kwenya majengo ya serikali. Utaona jina la maabara ya sayansi limechapishwa kwa Kiswahili kwanza na kuwekwa kwa Kiingereza kwenye mabano. Hapa kwetu, hatuweki jina la taasisi ama wizara kwa Kiswahili hata kwenye mabano. Tunachapisha tu kwa Kizungu bila Kiswahili. Tunafaa kuwa kwenye mstari wa mbele kuonyesha kuwa inawezekana kutumia Kiswahili kama lugha rasmi. Tunafaa kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika katika jamii. Tunapaswa tuwafunze watoto wetu pia. Haswa, sisi ambao ni wazazi wa watoto wachanga wanaopitia mfumo wa elimu wa CBC, ni jukumu letu kwenda shuleni kuona kwamba watoto wanafunzwa lugha ya Kiswahili. Tukishazaa watoto, kabla wafikishe umri wa kisheria wa kuenda shuleni, inafaa wawe wanapata mafunzo ya Kiswahili. Tunafaa kutumia Kiswahili katika jamii zetu kwa sababu lugha usiokuwa na uzoefu wa kuizungumza itapotea kwa sababu haitumiki. Kwa hivyo, ni jukumu letu kama wazazi kuhakikisha kwamba tunaitumia vizuri na tunawafunza watoto wetu ndio wakienda shuleni waweze kuendeleza mazungumzo na lugha zingine. Uzuri wa watoto ni wanaweza kujifunza lugha haraka. Hata ukizaa mtoto Uchina na umlete Kenya leo, atafunzwa Kiswahili na atashika kutoka mwanzo wake. Kwa hivyo, ni jukumu letu tuanze pale mwanzo. Tuko na wakati mzuri sasa kwa maana tuko na Baraza jipya la Mawaziri. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 21 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Mhe. Spika wa Muda, kama kuna jukumu moja muhimu ambalo Waziri aliyetwikwa jukumu hilo ako nalo saa hii, ni jukumu la kukuza Kiswahili humu nchini. Hivi sasa kuna jopo linalozunguka nchini kupokea maoni kutoka kwa washikadau kuhusu mfumo wa elimu wa CBC. Wakati utakapofika wa kuupiga msasa mtaala huu, tunafaa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili imechukua nafasi yake katika mpango wote wa elimu ya watoto wetu kuanzia PP1, ama gredi ya kwanza, ama elimu chekechea ndiyo mtoto akifika kiwango cha elimu ya juu awe ameifahamu vizuri lugha ya Kiswahili ndiyo hata akibahatika kuja Bungeni kama wanafunzi ambao wanatutembelea hapa, na kutazama mijadala, ajue kwamba Kiswahili ambacho watafunzwa pale mwanzo kwenye elimu chekechea, kwenye shule ya upili na hata kwenye chuo kikuu, ni kilekile Kiswahili ambacho kitatumika Bungeni. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, namuunga mkono Mhe. Yusuf na kumuhimiza kwamba asikomee hapa. Kwa sababu, kutokana na historia ya Bunge – mimi na wewe tumekuwa kwenye Mabunge ya 11 na 12, na sasa tuko katika Bunge la 13 – mengi ya maazimio tunayopitisha kupitia Miswada yanakwama wakati wa utekelezaji. Unabaki ukiyafuatilia kwenye Kamati ya Utekelezaji. Kwa hivyo, ninamhimiza Mhe. Yusuf kwamba ahakikishe kwamba pendekezo limeendelezwa hadi kuwa Mswada ili aulete Bungeni tuupitishe uwe sheria ndiyo suala hili liweze kupata uzito linalostahili na kutengewa bajeti kuhakikisha kwamba lengo letu limetimia. Hatuwezi kuwa tunasema tuko kwenye Umoja wa Afrika Mashariki bila ya kutekeleza maazimio ya umoja huo. Ukiaangalia Umoja wa nchi za Afrika, (AU) na UNESCO wameweza kukitambua Kiswahili. Lakini sisi wenyewe hatujaweza kubuni sheria ya kuliwesha jambo litendeke. Namhimiza Mhe. Yusuf kwamba, wakati hii Hoja itapitishwa katika na Bunge hili, asikwame hapo; angalie ni vipi tunawezakuendeleza mpaka iweze kuwa sheria ya nchi hii ndiyo tuwe kwenye msitari wa mbele kuhakikisha kwamba swala la kukikuza Kiswahili limewezekana. Mhe. Spka wa Muda, pia sisi, kama Wabunge, tujue kwamba tunapozungumza kuhusu usanifu wa lugha (grammar) kama alivyosema Mheshimiwa mmoja, tunapaswa kuzingatia kanuni zote za lugha. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Mhe. Martha, umekuwa na mabano mengi sana, na unasema tuzungumze Kiswahili sanifu. Mhe. Martha Wangari (Gilgil, UDA): Ninaifuata, Mhe. Spika wa Muda. Ndiyo maana ninaweka baadhi ya maneno kwenye mabano; haswa maneno ambayo ninayatoa kwenye lugha ya Kimombo. Nataka kusema kwamba tujihimize sisi wenyewe kama Wabunge, tuitumie hii lugha, sio hapa tu kwenye Bunge, lakini hata kwa nyumba zetu na kwa jamii zetu ili tuweze kupata uzoefu wa ulimi. Hii ni kwa sababu hata miongoni mwetu sisi Bunge, kuna wanaosema kwamba huu Mswada haueleweki vizuri. Hawajazowea mambo ya Kiswahili. Tukiendelea kuzungumza Kiswahili, tutapata uzoefu wa kuzungumza na hatimaye hata wanaotutazama, wakiwemo watoto, wajue kwamba Kiswahili ni lugha yetu sisi sote, na inatumika nchini kwote, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na vile vile katika Afrika nzima. Kwa hayo mengi, ninaiunga mkono Hoja hii. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Sasa twendeni Pwani, tumpate Bwana Bady Twalib kutoka Jomvu. Mhe. Bady Twalib (Jomvu, ODM): Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza nataka kumpongeza Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii. Nampongeza kwa sababu Mhe. Yusuf Hassan ni mheshimiwa mkakamufu ambaye tumefanya kazi naye katika Mabunge ya 11 na 12, na sasa tuko naye katika Bunge la 13. Kwa kuleta Hoja hili, ametufurahisha sana na pendekezo la kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa la Kiswahili humu nchini. Tunafahamu kwamba katika mwaka wa 1964, kule Tanzania, walibuni Baraza la Kitaifa la Kiswahili linaloitwa BAKITA. Vile vile, katika mwaka wa 1994, kule Zanzibar wakaunda baraza linaloitwa Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 22 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. BAKIZA. Tukiangalia katika kifungu cha saba cha Katiba ya Kenya, lugha mbili – Kizungu na Kiswahili – ndizo lugha rasmi humu nchini. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, pendekezo hili la kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa, kama alivyosema mwenzangu, Mhe. Martha, lisiwe Hoja pekee bali lifuatiliwe mpaka tubuni sheria kamili, na tuhakikishe kwamba Baraza hilo limetengewa bajeti yake. Vile vile, katika Bunge hili la 13, tusifanye mambo ya kawaida kama tulivyokuwa tukifanya katika Mabunge ya 12 na 11. Katika Mabunge yaliyopita, Hoja zinapitishwa lakini kutekelezwa inakuwa shida. Kwa hivyo, wakati huu ni muhimu Kamati ya Utekelezaji (Committee on Implementation) ihakikishe kwamba masuala yote yatakayopitishwa hapa yanatekelezwa. Mhe. Spika awa Muda, jambo hili la Kiswahili ni jambo ambalo litaweza kuunganisha Afrika Mashariki nzima. Tukiangalia nchini Tanzania, wanaongea Kiswahili. Waganda pia wanaongea Kiswahili. Na njia hii ya Kiswahili ndio itafanya iwe rahisi kwa watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya biashara na kuleta undugu. Tunajua kwamba hivi karibuni ndugu zetu wa kule Congo pia wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukiangalia Congo pia, watu wanazungumza Kiswahili. Ijapokuwa Kiswahili cha kule, kidogo ni tofauti na Kiswahili chetu. Kwa mfano, utamsikia Mkongo akisema, “Mimi nikiwa Papa Fulungenge, nasema kuwa batoto ba Congo na batoto ba Kenya, bote ni batoto bamoja.” Hivyo ndivyo Wakongo wanavyozungumza. Sote basi ni watu wamoja, Wakenya na vile vile Wakongo. Mhe. Spika wa Muda, kubuniwa kwa baraza hili la kitaifa kutaweza kufanya biashara na mawasiliano kuwa rahisi katika nchi hizi zetu. Tunaona katika Vifungu cha 119 na 137, vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vimewajibisha mataifa wanachama kustawisha na kuendeleza Kiswahili kama lugha ya mshikamano wa nchi wanachama. Kwa hivyo, Mheshimiwa, ukiangalia jambo kama hili limeweza kueneza ubora wa kuinua Kiswahili. Miongoni mwa jamii za Afrika Mashariki kuna lahaja mbali mbali za Kiswahili, ikiwemo Kijomvu, lakini hakuna Wajomvu. Mhe. Spika wa Muda, naona wafurahi, wacheka lakini wako Wajomvu. Mimi najifuharisha na nafurahi kuwa ni mmoja wa hao Wajomvu. Leo hii, utamuona Mswahili wa Kijomvu akitaka kutoa mfano wa watoto wawili ambao wanacheza na kwa bahati mbaya mmoja anamchoma kisu kwa jicho mwingine. Mjomvu husema, “Huyu mwana mkunzu unamtopoa,” yaani maana yake ni kuwa huyu ameweza kumkwaza mwingine kwenye jicho. Na vile vile, wakiogelea baharini, utawaskia wakisema, “Mwana huyu anaoga kutoka uta tauta katika pwani hii.” Kwa haya yote twajivunia kwa sababu hii ni lugha yetu. Na leo Kijomvu nakizungumza katika Bunge la Kenya. Kwa hivyo, ninafurahi kuwa Kijomvu ni moja ya lahaja za Kiswahili. Na punde, kama alivyosema… Ndipo ukaona Mhe. Martha akizungumza Kiswahili kidogo. Nilijua ni yeye kwa sababu uswahili ulikuwa umemnogea mpaka nikaona nikama ambaye anatoka Pwani. Ukienda Dar-es-Salaam, utapata kwamba katika maeneo mengi sana, hata kama kunawekwa mabango yoyote pale, utapata yanaandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Wanajivunia lugha yao ya Kiswahili. Mawasiliano mazuri yatainua biashara na ajira Afrika Mashariki. Hii ni kwa sababu ni Baraza zima ambalo linahitaji huduma kwa watu kulishughulikia. Nampongeza sana Mhe. Yussuf Hassan kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Nitakuambia mambo ya maajabu. Kati ya makabila madogo madogo 12 kule Mombasa, kuna makabila madogo ambayo kwa kimombo tunayaita minority tribes. Hayajulikani. Nataka kutaja katika kumbukumbu kwa kumpongeza kamishna mmoja wa polisi anayeitwa Murshid. Wakati uajiri wa polisi ulipofanyika katika sehemu yangu mwaka wa 2014, kuna mtoto mmoja wa Jomvu alitolewa kwa hesabu kwa sababu kabila yake haikuwa inajulikana. Nilipiga kelele kama Mbunge na nikafikisha barua kwa kamishna wa wakati ule. Ilidhibitika kuwa hiyo ndiyo moja katika kabila yenyeji ambayo inaishi sehemu hizo. Huyo mtoto alichukuliwa kama polisi. Leo hii anahudumia kitengo cha Kenya Police. Ni mtoto wa Mzee Salim. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 23 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Ni pongezi kwa Mhe. Yussuf Hassan kwa kuleta jambo njema. Sisi tunaotoka Pwani, ikiwa tumekuwa tukipata usingizi tukiwa tumejifunika blanketi nusu, leo tutajifunika blanketi nzima tukijua Kiswahili kinakombolewa nchini Kenya. Ahsante na Mwenyezi Mungu akubariki. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Vyema. Tuende kule Bonde la Ufa tumskize Bwana Francis Sigei kutoka Sotik, alafu atakayefuata ni Mhe. Lydia kutoka Taita Taveta. Mhe. Francis Sigei (Sotik, UDA): Mhe. Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kuchangia hii Hoja ya maana. Pia ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani kwa watu wangu wa Sotik walioona ni heri kunipatia fursa ya kuwahudumia. Nawapongeza. Baada ya kuwania hiki kiti mara tano, watu wa Sotik waliweza kunipa fursa hii. Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kuwahudumia wao. Leo ni siku ya maana sana kwangu kama mwakilishi wa Sotik kwa kuweza kuzungumza na Wakenya. Nikichangia huu mjadala, kwanza natoa shukrani za kipekee kwa Mhe. Yussuf Hassan. Najua yeye ni mkongwe. Ni mtu ambaye amefanya kazi nchini. Namtambua na nampa heshima. Namwona kama shujaa nchini kwa sababu ametetea tamaduni zetu. Mhe. Yussuf, tunakupongeza sana na Mungu akubariki. Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika nchi hii ni jambo la maana sana. Ningependa kuchukua hii nafasi kushukuru muanzilishi wa Taifa la Tanzania, Marehemu Nyerere, kwa kufanya jambo la maana sana. Alivyoanzisha utumizi wa lugha ya Kiswahili kwa nchi hiyo, alihakikisha wananchi wanaongea hiyo lugha. Tunajua kwamba umoja wa Tanzania ni dhabiti. Kuna Wakenya ambao wamechangia katika ubunifu wa lugha ya Kiswahili, mmoja wao akiwa marehemu Ali Mazrui aliyeandika vitabu. Pongezi kwake. Tungependa kuwa na watu kama hao. Jambo la maana kwa Baraza la Kiswahili ni kutoa mwelekezo, mikakati na namna ya kutumia lugha hii. Tungependa kulipatia nafasi hili kupanga hayo mambo. Tukipata baraza la Kiswahili, tutaweza kupata mwelekeo wa lugha ya Kiswahili. Naomba tushukuru wananchi wa Kenya. Wengi wanasubiri hii lugha iwe lugha ya taifa. Shida tuliyonayo ni mwelekeo na namna ya kutumia lugha sanifu. Lugha tunayoijua ni sheng. Mhe. Yussuf, tungependa uchukue hatua nyingine ili ulete Mswada. Lugha inayotumika mahakamani ni Kiingereza. Najua kwamba wanaohukumiwa wanahukumiwa bila kujua lugha iliyotumika. Wanaambiwa waaende jelani au wamepigwa faini halafu wakili wake anamueleza yaliyojiri. Inafaa tuanze kuchukua nafasi hii kama Serikali tuone kwamba lugha ya Kiswahili inatumika. Hata Kanuni za Kudumu tunafaa kuzitumia zile za lugha ya Kiswahili. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Mhe. Sigei, Kanuni za Bunge tayari ziko kwa lugha ya Kiswahili. Mhe. Francis Sigei (Sotik, UDA): Hatuzitumii. Ningependa lugha ya Kiswahili itumike siku moja kwa wiki katika hili Bungeni. Naunga mkono Hoja hii. Napongeza mashirika kama BBC na Sauti ya Marekani kwa kutusaida sana kwa kuendeleza lugha ya Kiswahili. Nakushukuru, Mhe. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hi ya Mhe. Hassan. Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’): Ahsante sana. Vyema. Tulisema kwamba nafasi hii ni ya Mhe. Haika. Mhe. Haika Mizighi (Taita Taveta, UDA): Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia fursa ya kuzungumza. Nimekuwa nikisubiri kwa muda ili nipate fursa hii hata mimi niweze kuchangia. Namshukuru Mwenyezi Mungu ya kwamba leo imefika. Pia nachukua fursa hii kuwashukuru watu wangu wa Taita Taveta kwa kunipatia kipindi cha pili ili niweze kuwatumikia kama kiongozi wao tena. Nawashukuru sana na nawambia kazi ile njema tulioweza kufanya, tutaifanya tena na zaidi. Nikirudi katika Hoja yetu ya leo, kwanza nampongeza sana Mhe. Yusuf Hassan kwa kuileta. Hoja hii ni bora sana na inasisitisa kuundwa kwa Baraza la Lugha ya Kiswahili. Kiswahili jamani kitukuzwe. Kiswahili ni lugha nzuri na imetambulika katika nchi yetu ya Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 24 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Kenya kama lugha ya Taifa. Kiswahili kama lugha ya Taifa katika nchi yetu ya Kenya haijatiliwa maanani. Hakijaheshimiwa kulingana na vile kimetambuliwa kama lugha ya Taifa. Kukibuniwa Baraza hili, basi, litaweka mikakati dhabiti ambayo itasababisha lugha hii yetu ya Kenya iweze kupendwa; iweze kuwa na watu wengi ambao wanaienzi na watu wanaojivunia lugha ya Kiswahili. Kiswahili ni lugha ambayo inaweza pia kutumika kuunganisha Wakenya. Tunajua vyema ya kwamba yako makabila mbalimbali lakini kuna jambo moja ambalo linaweza kutuunganisha. Lugha ni mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kuunganisha watu. Lugha ya Kiswahili inaweza kutuunganisha. Na sio Kenya pekee yake bali Africa nzima. Hata Africa Mashariki tunaweza kuunganishwa na lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii nikisema ni wakati wa usawa. Ya kwamba huu mpango mzima wa kubuni hili Baraza uweze kufanyika ili lugha hii iweze kutukuzwa katika Kenya nzima. Namshauri pia Mhe. Yusuf Hassan kwa kumueleza, baada ya hapa, tumekuwa tukizungumza hapa Bungeni na mara nyingi yanaishia hapa. Basi ni wakati tuweze kuenda hatua nyingine tena baada ya hapa tufuatilia yale tunayoyanena hapa tuyatende. Tuhakikishe kwamba lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu wanajivunia. Kuwe na mikakati bora na watu waweze kujifunza ili tuweze kuimarisha Kiswahili na kiwe bora katika nchi yetu na tuweze kuwa na Kiswahili cha kutuunganisha kama Wakenya. [Spika wa Muda (Mhe. David Ochieng’) aliondoka kwenye Kiti] [Spika wa Muda (Mhe. (Dr.) Rachael Nyamai) alikalia Kiti] Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa fursa hii na ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Pongezi kwa mheshimiwa aliyeleta Hoja hii. Ahsanteni sana. Spika wa Muda (Mhe. (Dr.) Rachael Nyamai): Ahsante Mbunge wa Taita Taveta. Anayefuata ni Mbunge wa Ganze ambaye ni Charo Kazungu. Mhe. Kenneth Tungule (Ganze, PAA): Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni yangu kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili hapa nchini Kenya. Pia nachukua fursa hii kumpongeza Mbunge wa Kamukunji, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili hapa nchini Kenya. Kama vile wenzangu wametangulia kusema, ni kweli kabisa kuwa Kiswahili ni lugha ambayo inadhaminiwa sana hapa Kenya na watu wengi. Ni lugha ambayo inatumiwa na makabila karibu yote hapa Kenya. Sio Kenya pekee yake, lakini ukiangulia ukanda wote wa Africa Mashariki, ukanda wote wa Maziwa Makuu na Afrika nzima kwa jumla, sasa wamekubali lugha ya Kiswahili na wameanza masomo mbalimbali katika nchi zao kuhakikisha kuwa lugha inabobea katika nchi hizo. Lakini la kushangaza hapa nchini Kenya bado tunachukulia lugha ya Kiswahili kama lugha dhaifu kwa sababu wengi wanafikiria mtu akiongea Kiswahili huwa hajasoma vizuri ama ana elimu duni. Wananchi wa Kenya huwa wanashabikia Kiingereza sana kuliko hii lugha yao ambayo imetambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya Kitaifa. Pale Pwani ninakotoka, lugha ya Kiswahili inakejeliwa sana, hata ukiangalia kwenye mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne. Ukiangalia vile wanafunzi wanavyofanya mitihani yao ya lugha ya Kiswahili, utapata hawapati alama nyingi sana ijapokuwa inasemekana wazi kwamba Pwani wanaongea Kiswahili. Lakini hali hii haionekani katika ile mitihani ya Kitaifa. Utapata wanaopita vizuri mtihani ya Kiswahili huwa ni shule za kutoka sehemu ya Bara wala siyo sehemu ya Pwani. Hili ni jambo ambalo ni lazima kama viongozi tulitilie maanani na ndio maana nasimama hapa kuunga mkono Hoja ya Mhe. Yusuf Hassan ya kusema ni lazima tubuni Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 25 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Baraza la Kitaifa ili tuweze kuhamasisha Wakenya tukijumuisha hata Wapwani ili waweze kuongea hii lugha na waweze kuisanifisha na kuongea kama vile ndugu zetu kule Tanzania tunawaona wakiongea. Hii lugha tukitumia vizuri inaweza kuunganisha Kenya. Tuna makabila zaidi ya 45 na kila kabila lina lugha yake. Tanzania wana makabila zaidi ya 50 lakini sio rahisi kujua Mtanzania ni wa kabila gani kwa sababu wote wameunganishwa na lugha ya Kiswahili. Naomba kama inawezekana, Baraza la Kitaifa hapa nchini liundwe ili liweze kuleta Wakenya wote pamoja ili waweze kusahau makabila yao, waweze kuwa na lugha moja ambayo itawaunganisha wote kama Wakenya. Mhe. Spika wa Muda, lugha ya Kiswahili haiongewi hapa Kenya pekee yake. Kama nilivyosema, hata Bara ya Ulaya na Uchina wanatumia Kiswahili. China wameandika walimu wengi wa Kiswahili wanaowafunza wananchi wao jinsi ya kuongea Kiswahili. Ukienda kule Marekani pia, utaona walimu wengi wa Kiswahili wamepelekwa huko. Wanafunza Wamarekani jinsi ya kuongea Kiswahili. Utaona kuna wasanii waliobobea Wamarekani ambao wameimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Michael Jackson aliwahi kuimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Lionel Richie pia aliimba wimbo katika lugha ya Kiswahili na hao ni Wamarekani. Msanii Rihana ameimba nyimbo katika lugha ya Kiswahili. Lakini hapa Kenya, sisi wenyewe tunadhalilisha lugha ya Kiswahili. Watu wanatoka nchi za mbali kuja Kenya kusoma lugha ya Kiswahili. Kuna wanafilamu waliobobea kutoka Marekani pia kama vile akina Forest Whitaker walikuja hapa Afrika, Uganda, wakasoma Kiswahili na wakatengeneza filamu kama vile The Last King of Scotland. Ni Wamarekani lakini wanaongea lugha ya Kiswahili na wanaongea Kiswahili sanifu. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan ya kuwa hapa Kenya pia tubuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kuhakikisha Wakenya wanaongea lugha sanifu. Hapa Nairobi najua kuna shida kubwa sana kwa sababu wanaingiza sheng kwa Kiswahili kila wakati. Wenyewe wanasema ni Kiswahili lakini mtu ambaye anatoka Pwani akisikia vile wanaongea pengine hataelewa hata neno moja ambalo linaongewa pale. Kiswahili kinaunganisha wananchi na kinaleta identity na uniformity. Hii itawezekena kama kutakuwa na baraza rasmi ambalo litakuwa linahakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inapewa kipaumbele. Inahitajika ili iweze kuwa lugha nzuri. Na sio lugha rasmi pekee yake, lakini pia iwe lugha nzuri ambayo inakubalika kila pembe zote za Kenya. Kwa hayo machache, ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Nazidi kupongeza hatua ya Mhe. Yusuf Hassan kwa kuhakikisha kuwa Baraza la Kitaifa ya Kiswahili litabuniwa hapa nchini Kenya. Ahsanteni sana. Spika wa Muda (Mhe. (Dr.) Racheal Nyamai): Mbunge wa Saboti, Caleb Luyai. Mhe. Caleb Amisi (Saboti, ODM): Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi mwafaka ya kujadili Hoja hii. Nampongeza rafiki yangu, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuwa na hekima ya kuleta Hoja kama hii. Lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimombo zimeorodheshwa kama lugha rasmi za kitaifa katika Katiba yetu ya Kenya. Lakini miaka kumi na miwili imeisha na hatujaweza kuitafsiri Katiba hiyo ikawa katika lugha ya Kiswahili vile ilivyo katika lugha Kimombo. Hicho ni kinaya - kwamba tumeiweka lugha ya Kiswahili kipao mbele katika Katiba ilhali hatujapata nafasi ya kutafsiri Katiba ya Kenya katika lugha ya Kiswahili. Nikikumbuka wale ambao wako na umri kama huu wangu ambao wametoka shule hivi majuzi, kuna vile vitabu tumesoma. Kuna wale ambao walibobea katika lugha ya Kiswahili na wakawa mstari wa mbele kukuza Kiswahili. Mfano ni yule aliyekuwa anatambulika, marehemu Ken Walibora. Wale wanakumbuka Ken Walibora - Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - alikua mstari wa mbele kuikuza lugha ya Kiswahili. Tulimpoteza na hakuna mahali tunamkumbuka. Ni vizuri tungekuwa tunawakumbuka watu kama hao ambao wamekuwa Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 26 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. mstari wa mbele. Wale wanaokumbuka kitabu cha Siku Njema, siku njema itakuja lini? Ni kitabu ambacho kilisifika sana kwa wale walikuwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule za upili. Ni kitabu ambacho kilibuniwa na kupaliliwa katika masomo na hata mtihani wa kidato cha nne. Unakumbuka pia tulikuwa na Wala bin Wala na yule aliandika kitabo cha wale ni sisi na sisi ni wale. Yaani Walenisi. Wanaokikumbuka hicho kitabu, kilikuwa na hekaya na riwaya ambayo ukiisoma unapata kusisimka na inasisimua akili yako. Kimeandikwa kwa njia ya kukejeli lakini kina mafunzo. Wale wanakumbuka hivi vitabu, vilitufunza mambo mengi tukiwa katika shule za upili na tulitahiniwa. Unakumbuka kulikuwa na wanafunzi wanapenda kusoma hivi vitabu na kufurahia. Lakini tukishamaliza mtihani, huo ndio ulikuwa mwisho wa Kiswahili. Hatuendelei kukuza lugha ya Kiswahili ili tuweze kuiweka mbele kama lugha ya kitaifa. Pia kuna kitabu ambacho kilijulikana kama Kitumbua Kimeingia Mchanga. Ni kitabu ambacho kilisifika sana. Hatujawahi kuwasifu wale wameandika vitabu hivi. Hatujawaweka mstari wa mbele. Tunaongea kuhusu kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya. Tungewaweka hao katika Baraza hilo ama kitengo cha kushughulikia maswala ya Kiswahili, na hivi tungeiweka Kiswahili mahali panapofaa. Mhe. Spika wa Muda, leo asubuhi nimekuwa na mkutano na raia wa Uingereza. Ingekuwa jambo kubwa kwamba huwezi kupata Mkenya akisema anasomea somo la Kiswahili. Lakini inanishangaza kwamba huyu Muingereza amekuja hapa hivi maajuzi, hajamalizia hata mwezi mmoja, lakini anakwambia: “Niko katika somo la Kiswahili. Najifunza lugha ya Kiswahili”. Itakuwaje kwamba wale wa nchi za ughaibuni wanatamani sana lugha yetu? Wanapofika hapa, jambo la kwanza wanalokuambia ni ‘naam’ na ‘ahsante’, kwa kuwa wameshajifunza. Wanajua kwamba ukifika Kenya, hata balozi anapotumwa Kenya, salamu za huko ni ‘ahsante’. Wameshajua kwamba Kenya na Kiswahili ni moja. Lakini sisi hapa hatuitambui lugha hii ila nchi nyingine zinaitambua lugha ya Kiswahili. Wao wana hamu sana ya kuisoma na kuingia shuleni wakitaka kufahamu hii lugha kwa undani. Hiki ni kinaya kikubwa sana. Pia, twafaa kuweka vyuo vikuu viwe na vitengo mwafaka vya Kiswahili ili wanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili, wajue mwishowe watapata kazi. Watasema tulikua tunaimba: ‘Someni vijana, mwisho wa kusoma mtapata kazi nzuri sana.’ Lakini sasa watu hawajui ikiwa watapata kazi baada ya kusoma. Watu wanajua baada ya kusoma ni giza na hakuna kazi. Sasa inafaa tujue kwamba tukiviweka vyuo vikuu vya kusomesha Kiswahili, wanafunzi watajua wakisoma somo hili la Kiswahili wataingia chuo kikuu na watakua walimu wa lugha ya Kiswahili. Chambilecho wahenga: Cha mkufuu mwanafuu ha, na akila hu; cha mwanafuu mkufuu hu, na akila ha. Ahsante sana. (Makofi) Spika wa Muda (Mhe. (Dkt) Racheal Nyamai): Ahsante sana Mheshimiwa. Nafasi inayofuata ni ya Mheshimiwa wa Turbo ambaye ni Mhe. Janet Sitienei. Mhe. Janet Sitienei (Turbo, UDA): Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Hoja hii. Kwanza kabisa napenda kumpa kongole Mheshimiwa wa Kamukunji kwa kuleta Hoja hii. Hakika, katika karne ya ishirini na moja, ni bora kutukuza lugha ya Kiswahili ili itumike sehemu zote nchini. Pia, sisi kama Wabunge twafaa tuwe na uzoefu wa kutumia lugha hii ya Kiswahili katika mijadala yetu. Hii ni ili wenye-nchi wetu - wakiwemo wazee, akina mama, vijana, pamoja na watoto - waweze kuelewa ni nini kinachoendelea bungeni. Nikitambua Kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinabainishia Serikali kulinda, kuendeleza ama kukuza matumizi ya Kiswahili, ningependa kuunga mkono Hoja hii ili iboreshwe kwa manufaa ya sisi wananchi wa Kenya. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 27 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Mkutano wa mwaka wa 2021 wa Marais wa Umoja wa Afrika Mashariki walikubaliana kubuni tume ya baraza la Kiswahili. Basi hatuna budi kuunga mkono kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kwa sababu hii itarahisisha wananchi kupata mawasiliano kamili. Pia itaboresha kufuzu kwa wanafunzi wetu wa kidato cha nne na kuingia chuo kikuu. Katika baadhi ya mahitaji ama masomo yanayohitajika kuingia chuo kikuu, wanaangalia sana lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa muda, kubuniwa kwa baraza hili kutasaidia zaidi. Nakumbuka wakati mmoja nilipigia mkaaji wa Mombasa simu. Nilipopiga simu, aliniuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa anamaanisha nini. Nilishinda nikimuambia: “Hapana! Mimi ni Janet!” Naye ananiuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa alimaanisha “ni nani anaongea”. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuweza kukuza lugha ya Kiswahili ili isaidie watu wengi. Itaboresha hata wanabiashara katika nchi ya Kenya. Kuna asilimia kubwa ya wanabiashara ambao hawawezi kuelewa ama kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwa hivyo kubuniwa kwa baraza hili itawawezesha kuweka mikakati bora ambayo itawasaidia wananchi wengi na kuwasaidia wafanyabiashara katika mawasiliano yao. Hivyo, uchumi wetu utakuzwa kupitia mawasiliano bora. Kubuniwa kwa baraza hilo kutachangia uhusiano, kuungana pamoja na mawasiliano bora kwa wenyeji wa Afrika Mashariki. Nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa Bungeni na mwenzangu Mhe. Yusuf, Mbunge wa Kamukunji. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangie. Spika wa Muda (Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Ahsante sana. Anayefuata ni Mhe. Nabwera Nabii, Mbunge wa Lugari. Alafu Mbunge wa Tigania Mashariki, Mhe. Mpuru Aburi. Inaonekana Mhe. Nabii ametoka kidogo. Kwa hivyo, tutaenda moja kwa moja kwa Mhe. Mpuru Aburi, Mbunge wa Tigani Mashariki. Mhe. Mpuru Aburi (Tigania East, NOPEU): Ahsante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kiswahili ni lugha ya maana sana kwa Wakenya wenzangu. Kwa sababu, ukiangalia kule mashinani, wakati tunakimbia huku na kule kuomba kura, hatutumii Kiingereza. Tunatumia Kiswahili. Siku hizi, hapa nchini Kenya, kila mtu ana runinga ndani ya nyumba yake. Lakini kule mashinani wanaoelewa Kiingereza ni wachache. Hata wenye pikipiki wakiwa na simu zao mkokoni husikiliza stesheni ya Bunge. Wabunge walikimbia huku na kule kuomba kura lakini hapa Bungeni, tunazungumza Kiingereza tu. Tukienda kunywa chai pale nje, hakuna yeyote anayeongea Kiingereza. Ni Kiswahili peke yake. Ndiyo maana naunga mkono ndugu yangu Bw. Hassan, kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hii ni kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuunganisha Wakenya ama mtu aliyesoma na yule hakusoma ila ni kupitia Kiswahili tu. Tukiangalia mambo ya mashamba, maofisa kutoka Wizara ya Lands yani makarani, huenda mashinani kushugulikia mambo ya mashamba. Wakifika huko, wanaongea Kiingereza tu hata katika kesi zote za mashamba. Mzee na mama hawaelewi; wanatingisha vichwa tu. Kumbe hapo wanakuliwa na hao makarani. Ndiyo nasema Kiswahili ni lugha ya maana sana. Ukiangalia wenzetu Watanzania, wanazungumza Kiswahili na kimewaunganisha wote. Mtanzania hajali kabila lake ni gani. Yeye anajua ni Mswahili na hawezi kuzungumza lugha nyingine ila Kiswahili tu. Lakini hapa nchini Kenya, ukienda kwenye ofisi za Serikali, unawapata watu wanazungumza Kiingereza. Hakuna lugha nyingine. Hata mtu akiwa anataka kuwaeleza kitu cha maana anashindwa, au kuskia aibu kwa sababu hatasikilizwa. Ukienda kortini au kwenye magereza kwa mfano Kamiti ama rumande huko Industrial Area, asilimia 80 ya wafungwa ni watu hawana makosa yoyote. Wakifika kortini, jaji, wakili na prosecutor wanazungumza Kiingereza. Sasa huyo jamaa anapanua mdomo tu mpaka anapelekwa ndani. Ndiyo maana naunga mkono Hoja hii ambayo itatupatanisha. Chama chetu cha National Ordinary People Empowerment Union (NOPEU), ni cha mwananchi wa kawaida. Sisi kama viongozi wa chama hiki lazima tuunge mkono Hoja hii ndiyo mwananchi wa kawaida aweze Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 28 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. kuinuka. Ni yule ambaye amekaliwa ama kufinyiliwa na wakoloni Waafrika wanaosema wanaelewa Kiingereza tu. Wakati umefika tupendane, tusikizane ili tuwe kitu kimoja kama Wakenya. Naunga Rais wetu mkono, kwa sababu wakati mwingine anaongea Kiingereza na akimalizia yale yote ameongea, anatafsiri kwa Kiswahili ndio mwananchi wa kawaida ambaye ni mzalendo na yule hustler aliyempigia kura afahamu alichosema. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Mimi hula miraa siku ya Ijumaa na nikila ‘veve’ zangu, tunaongea Kiswahili pale nyumbani na wenzangu. Hata saa hii tunapoongea, wale wanaokula miraa kule Meru na Mombasa… Mhe. Ndindi Nyoro (Kiharu, UDA): Hoja ya nidhamu, Mhe. Spika wa Muda. Spika wa Muda (Mhe. (Dkt.) Dr. Rachael Nyamai): Mhe. kuna hoja ya nidhamu kutoka kwa Mhe. Ndindi Nyoro. Mhe. Ndindi Nyoro (Kiharu, UDA): Mhe. Spika wa Muda, niko na hoja ya nidhamu. Hii ni kwa sababu katika sheria za Bunge ama Kanuni za Kudumu hufai kuchanganya lugha. Nimemskia Mhe. akiendelea kukuita Madam na kusema for example. Kuchanganya lugha ndio ningetaka... Hii ni kwa sababu, siku ya leo wanafunzi wengi wamefika hapa kututazama. Ni vizuri wakirudi shuleni wajue kuna nidhamu inayofaa ndani ya hili Bunge. Mhe. Mpuru Aburi (Tigania East,NOPEU): Ahsante Mhe. Spika wa Muda. … Spika wa Muda (Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Mhe. hakikisha unatumia lugha moja, halafu usirudie veve. Mhe. Mpuru Aburi (Tigania Mashariki, NOPEU): Ahsante Mhe. Naibu Spika. Mhe. Ndindi ni ndugu yangu mdogo mpendwa. Anajua wakati alipokuwa ameenda na maji kule, sikuruhusu abebwe na maji. Kwa hivyo, yeye hana maneno ya maana na si lazima aongee. Langu ni moja tu, kwamba naunga mkono Hoja hii ndiyo Kiswahili kienee hapa nchini na Wakenya wainuke. Nasema ahsante kwa watu wa Tigania Mashariki kwa kunipigia kura na kufanikisha kuja kwangu hapa Bungeni. Pia nasema ahsante kwa ndugu zangu waliokuwa katika Bunge lililopita kwa kunipigia kura ndiyo nikaenda East Africa Legislative Assembly (EALA). Mimi sina vita na mtu yeyote, naungana pamoja na Wakenya. Kama nilivyosema Kiswahili ni lugha ya maana. Sina mtoto wa mgongo au wa tumbo ama anayetoa makamasi, wote nitawaunganisha kama Wakenya. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga Hoja ya ndugu yangu mkono ndio Kenya yetu iendelee mbele. Thank you so much. Spika wa Muda (Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Ahsante Mheshimiwa. Tunapoendelea, ningependa kuwajulisha kwamba tuko na wanafunzi kutoka shule zifuatazo: Mugunda Girls High School, eneo Bunge la Kieni, Nyeri County; Nginda Girls High School, eneo Bunge la Maragwa, Murang’a Kaunti; St. Angela’s Girls High School, eneo Bunge la Kiambaa, Kiambu Kaunti na St. Regina Nairutia Mixed Secondary School, eneo Bunge ya Nyeri Mjini, Nyeri Kaunti. Karibuni katika Bunge. Anayefuata katika mazungumzo yetu ni Mhe. Joyce Kamene, Mbunge wa Machakos Kaunti. Atafuatwa na Mhe. John Kiarie. Mhe. Joyce Kamene? Hayuko hapa Bungeni na nilikuwa nimemuona? Kwa hivyo, tutaenda kwa Mhe. John Kiarie kutoka Dagoretti Kusini. Mhe. John Kiarie (Dagoretti Kusini,UDA): Nakushukuru sana, Mhe. Spika wa Muda. Siichukulii nafasi ya kuchangia Hoja hii kwa wepesi. Ningependa kwanza kumpongeza sana ndugu yangu ambaye pia ni Mjumbe wa Eneo Bunge lililo hapa mjini katika Kaunti ya Nairobi. Nampongeza sana Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya maana zaidi. Nafahamu kuwa Mhe. Yusuf Hassan ni mwanahabari anaye uzoefu mkubwa katika uhariri wa habari. Ni desturi na historia yake iliyomshawishi kuleta Hoja hii muhimu ya kutupendekeza tubuni Baraza la Kiswahili hapa nchini. Kwanza kabisa, nampongeza Mhe. Yusuf Hassan kwa wazo hilo bunifu na la maana zaidi kwa nchi yetu na lugha tukufu ya Kiswahili. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 29 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Mwimbaji wa wimbo aliimba na kusema Kiswahili kitukuzwe kwani ni lugha ya Taifa. Akasema pia watu wanapokutana bila lugha, watakwama. Hakika, chambilecho wahenga, mwacha mila ni mtumwa. Kunaye msomi tajika kwa jina la Leo Mohammed ambaye hufunza desturi za jamii, watu na mataifa. Katika mafunzo yake, mwalimu Leo Mohammed anatushawishi kwamba adui wa mtu ni mtu. Anatushawishi pia kuwa anayetaka kukutelekeza, kukupokonya na hata kukutia utumwani, jambo analofanya kwanza ni kukunyang’anya lugha yako. Mwalimu Leo Mohammed hufunza kwamba yeyote anayetaka kukufanya mtumwa, huwa kwanza anakunyang’anya jina la babako. Jina la babako ndilo hubeba asili yako. Kisha, anakunyang’anya lugha ya mamako kwa sababu hapo ndipo culture yako ipo. Hapo ndipo utamaduni wako upo. Anasema kwamba ni vizuri yeyote anayependa kuzingatia utamadani wake ahifadhi lugha yake. Nina hofu sana kwa sababu nchi yetu inatajika duniani nzima kwa sababu ya wanariadha wetu wanaotuletea sifa kuu. Lakini wanaposhinda na kukutana na wanahabari, huwa tunawaona wakijikanganya na lugha za kigeni. Wanapofanya hivyo, yule ambaye alikuwa amepata hadhi ya juu sana kwa kushinda mbio za riadha, anashushwa hadhi kwa sababu anajaribu kuongea kwa lugha ya kigeni. Anapojaribu kuongea lugha ya kigeni, anakanganywa na ile ambayo tunaita lafudhi – athari za lugha ya mama. Hii ni kwa sababu wengi wao wanatoka katika sehemu za Bonde la Ufa na Mlima Kenya. Wakijaribu kuongea lugha za kigeni, lafudhi inawatatiza, na wanapata athari kubwa sana za lugha ya mama. Napendekeza kuwa kupitia Baraza hili litakalobuniwa, tuwahimize wanariadha wetu kwamba lugha yao iwe ni Kiswahili. Yule ambaye anataka kumhoji ajifunze lugha yetu. Wagiriki wakishinda, wanaongea lugha yao. Wafaransa wakishinda, wanaongea Kifaransa. Huyo mwanahabari achukue jukumu la kutafsiri lugha yetu ili wanariadha wetu waweze kuhifadhi hadhi yao wakishinda mbio hizo. Wasishushe hadhi yao wakijaribu kuongea lugha zinazowatatiza. Ni jambo la kustaajabisha kwamba hapa nchini, tunaenzi mashirika na taasisi za kigeni ambazo zimebuni mabaraza ya lugha zao zilizo hapa nchini. Sio jambo baya kuwa na mabaraza hayo. Hapa Nairobi, tunazo British Council, Goethe Institute na Confucius Institute. British Council inaenzi lugha ya Kiingereza. Inaiimarisha na kuiweka katika safu za juu sana, na pia kutuhimiza tuongee lugha yao. Kwa hivyo, hili ni jambo la busara ambalo limeletwa hapa na Mhe. Yusuf. Tukiwa na taasisi yetu ambayo kazi yake ni kuhimiza watu waenzi lugha yetu, tutakuwa tumechukua hatua ya maana sana kama nchi. Pia, tutapeleka taasisi hiyo katika nchi za mbali ili tuhimize wananchi wakienzi Kiswahili. Tutakapobuni Baraza hili, itabidi tuwakumbuke wale magwiji wa lugha ya Kiswahili ambao walitutangulia. Kunao wasomi tajika. Tutaweza kumkumbuka msomi Ali Mazrui, aliyefanya kazi kubwa sana ya kuimarisha lugha ya Kiswahili na kueneza dini ya Kiislamu katika bara letu la Afrika. Tunahitaji mahali ambapo tunaweza kumuenzi msomi huyu. Kuna wasomi wa hivi punde kama vile Ken Walibora, ambaye vitabu vyake vilikuwa katika mtaala wa masomo ya nchi hii. Hatungependa kumsahau. Kando na wasomi, tuna watangazaji tajika kama Leonard Mambo Mbotela, ambaye ni gwiji wa lugha. Tunaye mwanahabari Swaleh Mdoe, na wengine wengi, ambao wameibuka kama watu tajika ambao wamemezea lugha yetu ya taifa. Baraza hilo la lugha ya Kiswahili lichukue jukumu hilo la kuwaenzi hao wasomi na magwiji wa lugha ya Kiswahili. Jambo lililonifadhaisha sana ni kuwa katika Kongamano la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wetu wa awali alikuwa Mwenyekiti katika kikao kilichopitisha hoja kuwa Kifaransa kijumuishwe katika lugha za nchi za Afrika Mashariki. Jambo hilo lilinifadhaisha sana kwa sababu katika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tuna lugha yetu ya kiasili ya Kiswahili. Hao tunaowaenzi zaidi na kutumia lugha zao, tusiwahi sahau hata siku moja kwamba walikuwa wakoloni waliotuweka utumwani. Kwa kuenzi lugha zao, tunaendeleza zile itikadi zao za kikoloni. Nahimiza Bunge hili lisimame kidete na kuiambia Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 30 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Jumuiya ya Afrika Mashariki ikosoe pendekezo hilo lililopitishwa kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitumie lugha ya Kifaransa kama mojawapo ya lugha rasmi. Tuinue Kiswahili mahali ambapo tulitaka kuweka lugha hizo za kigeni. Mwisho kabisa, kila mtu ana jukumu. Hata tunaposubiri Baraza hilo libuniwe ili tukuze lugha yetu, itatubidi sisi wenyewe tuchukue jukumu. Bunge hili litenge siku moja ya kujadiliana katika lugha ya Kiswahili. Tunazo Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Kwangu nyumbani, nimewahimiza watoto wangu wajue lugha ya kiasili ya mama na wanaiongea. Pia wanaiongea lugha ya Kiswahili. Wakienda shuleni, watafunzwa Kifaransa na Kizungu. Lakini nyumbani, mimi ni mwalimu wa kwanza wa lugha na nahimiza lugha zetu zienziwe daima na daima. Ahsante sana kwa kunipa nafasi hii, Mhe. Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwa lugha ya kitaifa tunayoienzi sana. Kiswahili kitukuzwe. Spika wa Muda (Mhe. (Dkt) Rachel Nyamai): Waheshimiwa Wabunge, naona watu wengi walikuwa na haja ya kuzungumzia Hoja hii, lakini muda ambao ulikuwa umetengewa umeisha. Ningependa kumuita Mtoa Hoja ahitimishe mjadala wake. Mhe. Yussuf. Mhe. Yusuf Hassan (Kamukunji, JP): Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Kwa sababu ya hamu kubwa imeonyeshwa na Wabunge, ningependa kuomba niwape Wabunge watatu ambao wameniomba wakati mdogo. Hao ni Mbunge wa Nandi, Cynthia Muge; Mbunge Rashid Bedzimba wa Kisauni; Mhe. Julius Sankuli wa Kilgoris; na Mheshimiwa wa eneo Bunge la Masinga. Naomba niwape hao wanne dakika moja moja ili waweze kuchangia. Spika wa Muda (Mhe. Rachel Nyamai): Katika orodha ambayo imetolewa na Mhe. Yusuf, tutaanza na Mhe. Cynthia. Mhe. Cynthia Muge (Nandi CWR, UDA): Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya umuhimu kabisa katika Bunge hili inayohusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili nchini Kenya. Kiswahili kama vile Wabunge wenzangu wamesema ni lugha ya maana sana ambayo inazungumzwa na watu wengi duniani. Naunga mkono Hoja hii nikisema kwamba tuhakikishe ya kuwa lugha ya Kiswahili imetukuzwa. Pia, pale kwenye Bunge za Kaunti, bado wanatumia Kanuni za Kudumu. Hawana chapisho kwa lugha ya Kiswahili. Hoja hii ni muhimu na itatusaidia sana. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kiasili ya Kiafrika na inatusaidia sisi kama Waafrika. Lugha ya Kiswahili ina heshima na hili Baraza litatusaidia tuhakikishe kwamba kila wakati tunadhibiti na kukuza lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Nashukuru Mhe. Yusuf kwa kunipatia hii nafasi niweze kuichangia na naiunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ahsante. Spika wa Muda (Mhe. Rachel Nyamai): Mhe. Bedzimba. Mhe. Rashid Bedzimba (Kisauni, ODM): Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kunipa hii fursa ili niweze kupenyeza sauti yangu katika Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Naunga mkono kwa sababu wakati Baraza hili litakapobuniwa, nina imani kwamba Kiswahili kitashamiri na kitakuwa lugha muhimu katika Taifa letu. Mataifa mengi yaliyondelea yalitumia lugha za mama. Ukiangalia Uingereza, Urusi na Bara la Arabu, wanatumia lugha zao na nchi hizo zimeendelea zaidi. Ukiangalia Taifa Jirani letu la Tanzania, limeweza kuwa na maendeleo mengi kwa sababu ya kutumia lugha zao. Ningeomba kwamba almashauri zote za kiserikali ziweze kuweka maandishi katika milango kwamba unapoingia katika jumba hili, unaweza kutumia lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kiswahili. Lugha ya Kiswahili si mawasiliano tu mbali lugha nzuri kwa Wakenya na Afrika Mashariki na haswa Pwani ambako ni kitovu cha Kiswahili. Lugha hii ni fursa ya vitu vingi. Spika wa Muda (Mhe. Rachel Nyamai): Mheshimiwa Sunkuli. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 31 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Mhe. Julius Sunkuli (Kilgoris, JP): Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan. Kungekuwa na mengi ya kusema lakini kwa kuunga mkono Hoja hii, ningependa tu kusema mambo mawili mafupi. Baraza la Kiswahili litakuwa na jukumu la kupa makaazi Kiswahili. Wakati huu hatujui Kiswahili kinahifadhiwa katika wizara gani. Ingekuwa ni Wizara ya Elimu lakini wengine wanasema ni Wizara ya Utamaduni. Baraza likija, tutajua ni nani atakua akikikuza Kiswahili. La mwisho, Baraza la Kiswahili litazawasisha Kiswahili na litatia muhuri Kiswahili sanifu hasa katika vyombo vya habari na pia vile viongozi walivyozungumza. Najua katika awamu ya… Spika wa Muda (Mhe. Rachel Nyamai): Mhe. Yusuf, malizia. Mhe. Yusuf Hassan (Kamukunji, JP): Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Leo tumekuwa na kikao cha kihistoria na naona kwamba tumefanikiwa katika kulizungumzia na tumekuwa na mjadala wa kusisimua. Tumekuwa na ari, mori na hamu kubwa sana ya kuweza kulizungumzia swala hili la Kiswahili. Tumetambua kwamba Kiswahili ni lugha muhimu ambayo ina hadhi na majukumu mbalimbali. Ni lugha ya kitaifa ambayo ni rasmi na ni lugha ya kimataifa. Ni dhahiri kwamba lugha hii ni muhimu sana na ina mawanda mapana ya kimatumizi kuliko lugha yoyote ya kiasili. Naomba tuipeleke mbele Hoja hii na ninataka kuweka swala hili mbele yako Mheshimiwa Spika wa Muda ili tuweze kuipeleka mbele katika Kikao kijayo. Nawashukuru wote ambao waliweza kuchangia na kulizungumzia. Nawapa hongera wanafunzi ambao wameweza kuhudhuria kikao cha kihistoria cha kwanza tangu niingie Bungeni. Nimekuwa katika Bunge la Kumi, Kumi na Moja na Kumi na Mbili. Ni mara ya kwanza ambapo tumetumia wakati mwingi kama huu kuzungumzia hii lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Spika wa Muda (Mhe. Rachel Nyamai): Ahsante Mhe. Yusuf Hassan. Waheshimiwa wa Bunge nitahairisha pendekezo la kutoa Hoja iamuliwe. Next Order.
Hon. John Kiarie.
Thank you, Hon. Temporary Speaker. I beg to move the following Motion: THAT, aware that there are many talents amongst the youth of this country; noting that these talents have been severally displayed through various inventions and also innovations by the artisans in platforms such as the Annual Youth Innovation Week and profiled on social media; concerned that most of those innovations and artworks do not go beyond making sensational stories in their localities, local dailies and social media mentions; noting that most of those innovations and artworks are crucial in ideas promotion, intellectual development and at creating employment and addressing the problems that affect us as Kenyans on a daily basis; concerned that there is inadequate support and administrative measures to support the artisans; cognizant of the fact that the Kenya Vision 2030 seeks to make our country an industrialized middle-income economy in the next nine (9) years; aware of the immense potential for wealth creation and job opportunities through our own local production generated if well-developed and commercialized; also recognizing that our imports are well in excess of Kshs2 Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 32 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. billion shillings and most of these imports are not relevant to the Kenyan market, noting that home-grown technology would be region-sensitive and appropriate for the environment, social economic dynamic and suitable for our utility; further concerned that most of those artisans lack appropriate technology, skills, capital and tools; this House resolves that the National Government, through the relevant Ministry, formulates a policy ring-fencing two per cent (2%) of the monies allocated under the National Government Constituencies Fund and UWEZO Fund for the purposes of equipping artisans with the necessary skills, technology and tools. I appreciate this opportunity to move this Motion. This is a Motion that is aimed at the empowerment of artisans by the National Government. This House is populated with Members of Parliament who have a responsibility of lobbying and oversighting the NG-CDF Fund which, at the moment, is limited to the functions of education, security, infrastructure and a bit of youth development through sports and conducive environment. The intent of this Motion is to persuade MPs to see it fit to expand the mandate of the NG-CDF to accommodate some skills development and facilitation of tools for our own hustlers who are struggling when they step out of training, apprenticeship and Technical and Vocational Education and Training (TVETs) institutions. When they step out of TVETs, they are not able to go into the market because they are deficient in skills and they do not have the tools and equipment that are required. I stand here to persuade my fellow MPs to see it fit for us to expand the mandate of the NG-CDF to cover those areas. Each one of us can tell stories from their constituencies of great innovations, skills and talents of young people who, if they were to be supported, they would end up going to the global stratosphere in terms of fame. Those skills exist in our country and many youths are talented. Young artists and artisans are doing wonders, but they have a limitation on start-ups. They are not able to step out of college and go into practice. So, if we expand the mandate of the NG-CDF to accommodate those artists by providing them with the necessary skills and tools, we will be equipping our young people to be fit for a time such as this. We are going to the technological world and digital age. We are going into an age where each and every person shall be remunerated for the ideas that they bring forth. They shall be remunerated commensurate to the problems that they are solving. The bigger the problem you solve, the bigger the pay. To equip our people for such a time as this, it will be in order for us to ask the NG-CDF patrons to expand its mandate to allow us to equip our own people; our young artists and artisans to live in this world. Hon. Deputy Speaker, we have a new Government. The Head of State made proclamations and he gave a vision for this country. When the Head of State sat where you are sitting, he stood up and gave us his vision for this country. Among the many things that the Head of State said were going to be the key pointers of his Government, is the creative and the digital economy. Also of importance is that the Head of State told us that he is seeking to get this country to digitalise and automate the operations of Government. Who are the people who will be digitalising and automating Government operations? If we are looking at moving to e- Government, who are the people who shall do that? It is our young people. By equipping them with skills and tools, we are enabling them to contribute to the development of this country as aligned in Vision 2030, the vision of Kenya Kwanza Government and the bottom-up approach. We will have the artists and artisans developing and pulling themselves by their bootstraps from the bottom. Kenya is a net importer of commodities. Some of them that land in this market are not fit for our environment and utility. The amount of plastic pollution in this country is chocking. We chock our soils and rivers and, in the process, we chock ourselves. If we equip our young people to manufacture toothbrushes, toothpicks, toilet and tissue papers, as well as serviettes Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 33 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. and many other small things that we use in this country, we shall prosper. We do not need to import things like cups, plates, tiles, fittings for our houses, lamp shades and bulbs. If we equip our young people with the necessary skills and tools that they need to innovate and develop, those are things that can be readily made in our counties and constituencies. Hon. Temporary Speaker, there was a big drive by the Deputy President who has now ascended to the Presidency, to construct Technical and Vocational Education and Training Institutions (TVETs) in our constituencies. They churn out graduates who find themselves like a deer in the headlights, when they land in the market and realise that despite being equipped with necessary training, they are unable to practise because they are limited by their skills and lack of tools. If we expand the mandate of the National Government – Constituencies Development Fund (NG-CDF) to cover skills training and tools provision, then we would have a ready industry for the graduates who come out of TVETs. Some of the technology that we import is not fit for this country. It is developed, but it specific to the region or areas where it emanates from. When it lands in Kenya, it has to be modified to be fit for this country. It is this time that we should now start developing appropriate technology for this country. I urge Members of Parliament to see the import in us equipping our young people with skills and tools. The Bible reminds us that when Moses was called, he said that he was not fit to lead the people. He said that he was a stammerer; unable to speak. The good Lord asked him what he had in his hands. He said he had a rod. He was told to take it and lead the people out of captivity into the promised land. For the people in Parliament, the rod or stuff that they hold is the NG-CDF. Even as we, Members of Parliament, urge Government ministries and the Executive for policies, we can take the first step in faith by using what is in our control and hands to start walking towards a journey of equipping our young people with skills and required tools, so that they can offer appropriate technology that is fit for a time such as this in the history of our country. We are speaking about the future. We call ourselves to be alert that we are now in the fourth industrial revolution where Africa can leapfrog to the front. We were borrowers of technology in the first, second and third industrial revolutions. However, in the fourth industrial revolution, Kenya is known to have invented financial technology that is acclaimed globally. We invented M-Pesa which is heralded and glorified as one of the finest inventions of our time. How about we develop more young people who can give us more M-pesas and innovations for the future? Hon. Temporary Speaker, I take this opportunity to urge Members of Parliament to support this Motion. Because my time is up, I would like to request for your guidance because Hon. Professor is ready to second this Motion. I will seek guidance from you as to whether she will second it now or in the afternoon. Thank you very much, Hon. Temporary Speaker.
Thank you, Hon. Kiarie. That will be done in another sitting. (Seconding of the Motion deferred)
Hon. Members, the time being 1.00 p.m., this House stands adjourned until this afternoon at 2.30 p.m. The House rose at 1.00 p.m. Novemba 2, 2022 MIJADALA YA BUNGE LA TAIFA 34 Ilani: Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu. Published by Clerk of the National Assembly Parliament Buildings Nairobi